Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)
KATIBU MKUU WA UVCCM, NDUGU HALID MWINYI, APOKELEWA MKOANI ARUSHA | UVCCM
KATIBU MKUU WA UVCCM, NDUGU HALID MWINYI, APOKELEWA MKOANI ARUSHA | UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)
Habari Nyingine

KATIBU MKUU WA UVCCM, NDUGU HALID MWINYI, APOKELEWA MKOANI ARUSHA

13 Feb, 2026 00:00 Admin User 50 views 0 comments
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM)  na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Ndugu Halid Mwinyi, leo tarehe 13 Februari 2026, amepokelewa  katika Ofisi za UVCCM Wilaya ya Arusha Mjini, mkoani Arusha.
Mapokezi hayo yalihudhuriwa na viongozi wa UVCCM Mkoa wa Arusha, viongozi wa wilaya, vijana wa Chama pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo.
Mara baada ya kuwasili, Ndugu Mwinyi alipata fursa ya kusalimiana na vijana, kukagua mazingira na miundombinu ya ofisi, pamoja na kupokea taarifa ya kina kuhusu utekelezaji wa mipango, programu na mikakati ya jumuiya katika Wilaya ya Arusha Mjini. 
Akiwa mkoani Arusha, Ndugu Mwinyi pia anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika Baraza la Kawaida la UVCCM Wilaya ya Arusha Mjini, pamoja na kushiriki katika hafla ya kuwakaribisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza (Welcome First Year) katika Chuo cha Institute of Accountancy Arusha (IAA) – Main Campus.

#KazinaUtuTunasongaMbele
#FutureBilaStresi
Admin User

Mwandishi wa UVCCM - Anatoa taarifa za kusisimua kuhusu shughuli za vijana na maendeleo ya taifa.