Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)
DKT. MIGIRO AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA NAMIBIA, WAJADILI KUIMARISHA URAFIKI WA KIDUGU | UVCCM
DKT. MIGIRO AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA NAMIBIA, WAJADILI KUIMARISHA URAFIKI WA KIDUGU | UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)
Habari Nyingine

DKT. MIGIRO AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA NAMIBIA, WAJADILI KUIMARISHA URAFIKI WA KIDUGU

12 Feb, 2026 00:00 Admin User 40 views 0 comments
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro, leo Alhamisi, Februari 12, 2026, amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Namibia nchini Tanzania, Mheshimiwa Gabriel Pandureni Sinimbo.
Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi Ndogo ya CCM, Lumumba, jijini Dar es Salaam, yakihusisha masuala ya kimkakati yanayolenga kuimarisha ushirikiano wa kihistoria na mahusiano ya kidugu kati ya CCM na Chama cha SWAPO cha Namibia, ambacho kwa muda mrefu kimekuwa mshirika wa karibu wa kisiasa na kiitikadi wa CCM tangu enzi za harakati za ukombozi wa Bara la Afrika.
Katika kikao hicho, viongozi hao wawili wamejadili namna ya kuendeleza ushirikiano katika nyanja za kisiasa, kiitikadi, diplomasia ya vyama, pamoja na kubadilishana uzoefu katika uongozi na maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Aidha, wameweka msisitizo juu ya kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Namibia, kwa kuzingatia misingi ya mshikamano wa kihistoria, heshima ya pande zote, na ajenda ya maendeleo endelevu ya Afrika.
Admin User

Mwandishi wa UVCCM - Anatoa taarifa za kusisimua kuhusu shughuli za vijana na maendeleo ya taifa.