Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)
KATIBU MKUU WA UVCCM KUONGOZA KIKAO CHA SEKRETARIETI YA BARAZA KUU LA UVCCM, ZANZIBAR | UVCCM
KATIBU MKUU WA UVCCM KUONGOZA KIKAO CHA SEKRETARIETI YA BARAZA KUU LA UVCCM, ZANZIBAR | UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)
Habari Nyingine

KATIBU MKUU WA UVCCM KUONGOZA KIKAO CHA SEKRETARIETI YA BARAZA KUU LA UVCCM, ZANZIBAR

09 Feb, 2026 00:00 Admin User 153 views 0 comments
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Ndugu Halid Mwinyi (MNEC), anatarajiwa kuongoza kikao cha Sekretarieti ya Baraza Kuu la UVCCM kitakachofanyika Jumanne, tarehe 10 Februari 2026, katika Chuo cha Umoja wa Vijana Tunguu, Zanzibar.
Kikao hicho kitaanza rasmi kuanzia saa 8:00 mchana, na kinatarajiwa kujadili masuala muhimu ya kiutendaji, kimkakati pamoja na mwelekeo wa jumla wa utekelezaji wa majukumu ya UVCCM kwa kipindi husika.
UVCCM, kama jumuiya yenye dhamana ya kuandaa, kuunganisha na kuongoza vijana wa Kitanzania kisiasa, imeendelea kusimamia shughuli zake kwa kuzingatia misingi ya uongozi wa vikao, uwajibikaji na maamuzi ya pamoja
Admin User

Mwandishi wa UVCCM - Anatoa taarifa za kusisimua kuhusu shughuli za vijana na maendeleo ya taifa.