UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

UVCCM MBEYA MJINI YAADHIMISHA MIAKA 49 YA CCM KWA SHUGHULI ZA KIMAENDELE MBEYA MJINI

31 Jan, 2026 15 Machapisho
Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Mbeya Mjini ameshiriki leo katika shughuli za kimaendeleo katika Kata ya Nzovwe, pamoja na Diwani wa kata hiyo.
Shughuli zilizofanyika ni pamoja na kukarabati barabara na kujaza vifusi katika maeneo korofi, hatua zilizolenga kuboresha miundombinu ya wananchi na kuendeleza huduma za kijamii.
Maadhimisho haya yamefanyika sambamba na kuadhimisha miaka 49 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), huku UVCCM ikisisitiza dhamira yake ya kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kuendeleza maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa wananchi.