UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

Arusha: Mwenyekiti UVCCM Mkoa Simon Maximilian aongoza Maadhimisho ya Miaka 49 ya CCM

31 Jan, 2026 8 Machapisho
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Arusha, Simon Maximilian, awaongoza vijana wa umoja huo katika maadhimisho ya kuelekea miaka 49 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakionesha uzalendo kwa kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii na za chama.

Vijana hao wametembelea mashina ya chama katika eneo la Nduruma mkoani Arusha na kusimika bendera za CCM katika nyumba za mabalozi, wakisisitiza nafasi muhimu ya balozi kama kiungo cha msingi kati ya chama na wanachama wa ngazi ya chini.

Akizungumza wakati wa shughuli hizo, Maximilian anasema mabalozi ni nguzo muhimu ya chama kwani wanachama wote huanzia ngazi ya shina, hivyo wanastahili kutambuliwa na kuenziwa.

Mbali na shughuli za kichama, maadhimisho hayo yanaambatana na upandaji miti na ukabidhi wa miche miambili katika Hospitali ya Nduruma, tukio linaloonyesha dhamira ya vijana wa UVCCM kuunga mkono utunzaji wa mazingira na kusaidia jamii. Miche hiyo imekabidhiwa hospitalini kama sehemu ya juhudi za kurejesha na kuimarisha huduma za mazingira.

Maadhimisho haya yanathibitisha jitihada za UVCCM kuendelea kuenzi historia ya chama, kuenzi waanzilishi wake, na kushirikisha vijana katika malengo ya maendeleo ya taifa.