UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

KATIBU MKUU WA UVCCM ASHIRIKI DUA MAALUM YA KUMUOMBEA RAIS DKT. SAMIA

26 Jan, 2026 26 Machapisho
Zanzibar | Januari 26, 2026

Katibu Mkuu wa UVCCM na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Ndugu Halid Mwinyi, ameshiriki katika dua maalum ya kumuombea kheri Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, wakati wa kumbukizi ya siku yake ya kuzaliwa iliyoandaliwa na Afisi Kuu ya UVCCM Zanzibar.
Dua hiyo iliambatana na chakula cha pamoja na watoto yatima 800, tukio lililoonesha upendo na mshikamano kwa jamii. Aidha, dua hiyo ni ishara ya shukrani kwa kiongozi anayejali maendeleo ya Taifa na fursa kwa vijana.
Rais Dkt. Samia amekuwa kiongozi wa mfano, anayejali sana vijana na maendeleo ya Taifa zima, jambo ambalo limechochea mshikamano na matumaini kwa wananchi  wote .
Hafla ya kumbukizi ya siku ya kuzaliwa ya Rais ilijaa furaha, mshikamano na matumaini, ikionyesha kwa vitendo jinsi kiongozi anavyopendwa na kuthaminiwa na wananchi wake.
#HappyBirthdayDktSamia