UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

DIWANI LUTFIA AONGOZA WANANCHI KUFANYA USAFI WA MAZINGIRA

25 Jan, 2026 40 Machapisho
Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa kutoka Mkoa wa Mjini Unguja, ambaye pia ni Diwani wa Wadi ya Kwahani, Ndugu Lutfia Juma Idd, ameongoza wakazi wa wadi hiyo kushiriki zoezi la usafi wa mazingira lililofanyika katika maeneo mbalimbali ya wadi hiyo.
Zoezi hilo lililoshirikisha wananchi wa makundi tofauti limejikita katika kusafisha mitaa, maeneo ya wazi na mazingira yanayozunguka makazi ya wananchi, likiwa na lengo la kuimarisha afya ya jamii, kuzuia magonjwa ya mlipuko na kuendeleza utamaduni wa uwajibikaji wa pamoja katika kulinda mazingira.

Kwa upande wake, Umoja wa Vijana wa CCM chini ya Mwenyekiti wake, Ndugu Mohammed Ali Kawaida (MCC), umeendelea kudhihirisha dhamira ya dhati ya kushiriki moja kwa moja katika shughuli za kijamii zenye kugusa maisha ya wananchi, ikiwemo usafi wa mazingira, uhamasishaji wa uzalendo na kuchochea maendeleo endelevu katika jamii.
UVCCM imeendelea kuwa chachu ya mshikamano wa vijana na wananchi kwa ujumla.
#kazinaututunasongambele
#fyuchabilastresi