UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

VIJANA: TUPO TAYARI KUZIPOKEA FURSA ALIZOTUANDAA DKT. SAMIA” – VIJANA DODOMA

24 Jan, 2026 20 Machapisho
Dodoma. Maelfu ya wanafunzi kutoka vyuo vya kati na vyuo vikuu wamejitokeza kwa wingi leo tarehe 24 Januari, 2026 katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma, kushiriki Kongamano la UNI-Summit Life In & After Campus, linalolenga kuwajengea vijana uelewa wa kina kuhusu fursa mbalimbali zilizopo Serikalini na katika sekta binafsi.
Kongamano hilo limekusudia kuwaandaa vijana tangu wakiwa vyuoni na hata baada ya kuhitimu masomo yao, kwa kuwapatia elimu ya vitendo kuhusu ajira, ujasiriamali, ununuzi wa umma, ubunifu, TEHAMA na sera mbalimbali zinazolenga kumkwamua kijana kiuchumi na kijamii.

TUPO TAYARI KUZIPOKEA FURSA ALIZOTUANDAA DKT. SAMIA” – VIJANA DODOMA
Hamasa ya vijana hao ni dhahiri kwamba “wapo tayari kuzipokea na kuzitumia ipasavyo fursa alizowaandalia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan”, hususani katika awamu ya Sita inayosisitiza kazi na utu pamoja na maendeleo jumuishi 
Kupitia mijadala na mada mbalimbali, vijana wamepata nafasi ya kuelewa sera, mikakati na programu za Serikali pamoja na taasisi binafsi zinazolenga kuwawezesha kujiajiri, kuajiriwa na kushiriki kikamilifu katika uchumi wa taifa.

Kongamano la UNI-Summit Life In & After Campus limeandaliwa na Seneti ya UVCCM Mkoa wa Dodoma, likiwa ni sehemu ya mkakati wa kuandaa vijana kuwa wazalendo, wabunifu na washiriki hai wa maendeleo ya taifa.
Mgeni rasmi katika kongamano hilo ni Mwenyekiti wa UVCCM Taifa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Ndugu Mohammed Ali Kawaida, ambaye anatarajiwa kutoa mwelekeo na msukumo kwa vijana juu ya matumizi sahihi ya fursa zinazotolewa na Serikali.
Kongamano hilo ni jukwaa muhimu la kuunganisha elimu, sera na vitendo, likiwaandaa vijana kwa maisha ya chuo na baada ya chuo katika kujenga Tanzania yenye maendeleo jumuishi.
#KaziNaUtuTunaSongaMbele
#UniSummitLifeInAndAfterCampus