UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

KAWAIDA AWASILI PEMBA KUFUNGA MATEMBEZI YA MAADHIMISHO YA MIAKA 62 YA MAPINDUZI MATUKUFU YA ZANZIBAR

08 Jan, 2026 41 Machapisho
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Ndugu Mohammed Ali Kawaida, amewasili katika Kisiwa cha Pemba kwa ajili ya kuongoza na kufunga matembezi ya maelfu ya vijana kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Miaka 62 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Matembezi hayo makubwa ya kihistoria yanatarajiwa kufanyika Ijumaa tarehe 09 Januari, 2026, katika Mkoa wa Kusini Pemba, yakihusisha vijana kutoka maeneo mbalimbali wakionesha mshikamano, uzalendo na utii kwa misingi ya Mapinduzi Matukufu yaliyoleta uhuru, haki na maendeleo kwa wananchi wa Zanzibar.

Ndugu Kawaida, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MCC), ataongoza matembezi hayo kama sehemu ya kilele cha maandalizi ya maadhimisho ya Mapinduzi, akisisitiza umuhimu wa vijana kuendelea kulinda amani, umoja na mafanikio yaliyopatikana tangu mwaka 1964.