UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

ZIARA YA KATIBU MKUU CCM DKT.ASHA -ROSE MIGIRO, KUKUTANA NA MABALOZI WA SHINA WA CCM

07 Jan, 2026 90 Machapisho
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Asha Rose Migiro, ameanza ziara yake ya kikazi katika Mkoa wa Dar es Salaam kwa kukutana na kuzungumza na mabalozi wa mashina ya CCM, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa uongozi wa chama wa kuimarisha utendaji kuanzia ngazi ya chini.
Akizungumza kupitia ukurasa wake rasmi wa mtandao wa kijamii wa Instagram, Dkt. Migiro ameandika:
“Leo nimeanza ziara yangu katika Mkoa wa Dar es Salaam kukutana na kuzungumza na mabalozi wa shina wa Chama Cha Mapinduzi. Ni ari yangu kujua na kufahamu mipango kazi iliyopo kwenye mashina yetu.”
Kupitia ziara hiyo, Katibu Mkuu huyo analenga kusikiliza kwa karibu hali halisi ya uendeshaji wa shughuli za kichama katika mashina, kufahamu mipango waliyojiwekea mabalozi pamoja na changamoto zinazowakabili katika kukijenga, kukilinda na kukikuza Chama Cha Mapinduzi katika jamii.
Ziara ya Dkt. Asha Rose Migiro katika Mkoa wa Dar es Salaam inaakisi dhamira ya dhati ya uongozi wa CCM ya kushuka chini, kuzungumza moja kwa moja na wanachama na kuimarisha mshikamano wa chama kuanzia ngazi ya shina hadi Taifa, hatua inayotarajiwa kuongeza ari ya utendaji na uwajibikaji miongoni mwa mabalozi na wanachama wa CCM.