UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

Rais Samia Afanya Mazungumzo na Viongozi wa Wizara ya Ulinzi

06 Jan, 2026 36 Machapisho
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya mazungumzo na Viongozi wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa katika Ikulu ndogo ya Tunguu, Zanzibar, tarehe 06 Januari, 2026. Mazungumzo hayo yalilenga kujadili masuala mbalimbali ya ulinzi, usalama wa taifa pamoja na mchango wa Jeshi la Kujenga Taifa katika maendeleo ya nchi.

Baada ya kumalizika kwa mazungumzo hayo, Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliagana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Jacob John Mkunda, ikiwa ni sehemu ya ratiba ya shughuli rasmi za kiserikali zilizoendelea Ikulu ndogo ya Tunguu.

Katika hatua nyingine, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan  alipata wasaa wa kupiga picha ya pamoja na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Rhimo Simeon Nyansaho, Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Balozi Dkt. Moses Kusiluka, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Faraji Mnyepe, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Jacob John Mkunda, pamoja na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele. Tukio hilo lilifanyika mara baada ya kukamilika kwa mazungumzo hayo Ikulu ndogo ya Tunguu, Zanzibar