UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

MATEMBEZI YA MAADHIMISHO YA MIAKA 62 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR YAANZA RASMI MKOA WA MJINI MAGHARIBI

06 Jan, 2026 230 Machapisho
Matembezi ya kuadhimisha Miaka 62 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yameanza rasmi leo katika Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja, yakihusisha makundi mbalimbali ya vijana, wanachama wa Chama Cha Mapinduzi pamoja na wananchi, waliokusanyika kuonesha mshikamano, uzalendo na heshima kwa historia ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Matembezi hayo yanafanyika chini ya mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Ndugu Khalid Mwinyi(MNEC), ambaye anaongoza vijana na wanachama wa chama hicho katika kushiriki shughuli hiyo muhimu ya kitaifa yenye lengo la kuenzi misingi, tunu na mafanikio ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Maadhimisho ya Miaka 62 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanaendelea kuwa nyenzo muhimu ya kuimarisha umoja wa kitaifa, mshikamano wa vijana na kukuza elimu ya uzalendo, huku yakikumbusha mchango mkubwa wa Mapinduzi katika kujenga Zanzibar ya amani, maendeleo na ustawi wa wananchi wake.