JESSICA MSHAMA AONGOZA MATEMBEZI YA HAMASA MULEBA
15 Oct, 2025
22 Machapisho
Katibu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi wa UVCCM Taifa, Ndg. Jessica Mshama, ameongoza matembezi ya maelfu ya vijana wa hamasa wilayani Muleba, mkoani Kagera, leo tarehe 15 Oktoba 2025, kuelekea kwenye mkutano wa hadhara wa Mgombea wa Urais wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Vijana hao walishiriki kikamilifu katika matembezi hayo na kwa hamasa ya pamoja, wakionyesha imani yao kubwa kwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan na mchango wake katika maendeleo ya Muleba. Ndg. Jessica Mshama aliwataka vijana wote kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa Oktoba 29, 2025, kuhakikisha wanatiki kwa kishindo kumchagua Mgombea wa Urais, pamoja na wagombea wa CCM katika nafasi za ubunge na madiwani.
Matembezi haya yamethibitisha mshikamano wa vijana, dhamira yao ya kushiriki uchaguzi kwa amani na utulivu, na kujitolea kwa maendeleo endelevu ya taifa.
✅ #OktobaTunaTiki
✅ #FyuChaBilaStresi
✅ #TokaNiTokeTukaTiki
Habari Zinazohusiana
KURA YANGU SAUTI YANGU
26 Oct, 2025
Ni haki yangu kushiriki Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, 2025
KAWAIDA: "WATAKE WASITAKE CCM ITASHINDA KWA KISHINDO KIKUBWA TAREHE 29"
26 Oct, 2025
Mwenyekiti wa jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa komredi Mohammed Ali Kawaida akizungumza na wananchi walio jitokeza kwa wingi katika Ufungaji wa Kampeni Jimbo la Chaani Mkoa wa Kaskazini Unguja.
MARTINE AHAMASISHA WAPIGA KURA KUBEBA KADI ZAO OKTOBA 29 NA KUTIKI KWA DKT. SAMIA SULUHU HASSAN
26 Oct, 2025
Dar es Salaam, Oktoba 25, 2025 Mkuu wa Idara ya Uhusiano wa Kimataifa wa Vyuo na Vyuo Vikuu Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Ndg. Emanuel Martine, amewahamasisha wafanyabiashara, wajasiriamali, wateja na wadau mbalimbali wa Soko la Mabibo jijini Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi kupiga kura tarehe 29 Oktoba 2025, wakichagua kwa kishindo wagombea wote wa CCM.