MKUU WA MKOA WA SONGWE AFURAHISHWA NA UBUNIFU WA UVCCM KUPITIA MFUMO WA “KIJANI ILANI CHATBOT
15 Oct, 2025
18 Machapisho
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mheshimiwa Jabiri Omari Makame, ametembelea banda la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) katika Maonesho ya Wiki ya Vijana Kitaifa yaliyotamatika katika Viwanja vya Uhindini Jijini Mbeya leo tarehe 14 Oktoba 2025 na kutoa pongezi kwa ubunifu wa kidijitali uliofanywa na vUVCCM chini ya uongozi bora wa Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Ndugu Mohamed Ali Kawaida (MCC).
Akizungumza baada ya kutembelea banda hilo, Mheshimiwa Makame ambaye pia aliwahi kuwa Mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Taifa (2012–2015) amepongeza mfumo wa kisasa wa “Umoja wa Vijana wa Ilani ya CCM Kijani Ilani Chatbot”, akisema ni njia bora na ya ubunifu wa habari na mawasiliano inayowawezesha vijana kujifunza kuhusu utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020–2025 na kujua malengo ya Ilani ijayo ya CCM 2025–2030 kwa urahisi zaidi kupitia teknolojia.
Ameeleza kuwa Kijani Ilani Chatbot ni mfano wa mwelekeo mpya wa UVCCM katika kutumia TEHAMA kama nyenzo ya elimu, ushirikishwaji, na mawasiliano.
Makame ameongeza kuwa: “Msingi wa Mwenge wa Uhuru ni Umoja wa Vijana wa CCM, na ndiyo maana nembo ya UVCCM ina Mwenge wa Uhuru.”
KAULI MBIU:
💪 NGUVU KAZI YA VIJANA KWA MAENDELEO ENDELEVU
SHIRIKI UCHAGUZI MKUU 2025 KWA AMANI NA UTULIVU
#KazinaUtuTunasongaMbele ✅
#TokaNitokeTukatiki ✅
#OktobaTunatiki ✅
#TunazimazoteTunawashaKijani ✅
Habari Zinazohusiana
KURA YANGU SAUTI YANGU
26 Oct, 2025
Ni haki yangu kushiriki Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, 2025
KAWAIDA: "WATAKE WASITAKE CCM ITASHINDA KWA KISHINDO KIKUBWA TAREHE 29"
26 Oct, 2025
Mwenyekiti wa jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa komredi Mohammed Ali Kawaida akizungumza na wananchi walio jitokeza kwa wingi katika Ufungaji wa Kampeni Jimbo la Chaani Mkoa wa Kaskazini Unguja.
MARTINE AHAMASISHA WAPIGA KURA KUBEBA KADI ZAO OKTOBA 29 NA KUTIKI KWA DKT. SAMIA SULUHU HASSAN
26 Oct, 2025
Dar es Salaam, Oktoba 25, 2025 Mkuu wa Idara ya Uhusiano wa Kimataifa wa Vyuo na Vyuo Vikuu Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Ndg. Emanuel Martine, amewahamasisha wafanyabiashara, wajasiriamali, wateja na wadau mbalimbali wa Soko la Mabibo jijini Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi kupiga kura tarehe 29 Oktoba 2025, wakichagua kwa kishindo wagombea wote wa CCM.