Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)
KARDO International Street Culture & Sport Competition 2026 – Fursa ya Kuiwakilisha Tanzania Nchini Urusi | Fursa za Vijana | UVCCM

KARDO International Street Culture & Sport Competition 2026 – Fursa ya Kuiwakilisha Tanzania Nchini Urusi

Fursa Nyingine Maombi yameisha
11
Wameona
KARDO International Street Culture & Sport Competition kwa kushirikiana na Kituo cha Sanaa na Utamaduni cha Urusi nchini Tanzania
Shirika
Vladivostok, Urusi
Mahali

Maelezo ya Fursa

Vijana wa Tanzania wanakaribishwa kutuma maombi ya kushiriki katika KARDO International Street Culture & Sport Competition 2026. Mashindano haya yanawakutanisha vijana wenye vipaji katika sanaa za mitaani na michezo ya kisasa kutoka mataifa mbalimbali duniani. Hii ni fursa ya kuonyesha uwezo wako, kujifunza, kujenga mtandao wa kimataifa na kuiwakilisha Tanzania katika jukwaa la dunia.
FURSA YA KIMATAIFA KWA VIJANA WA TANZANIA πŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ‡·πŸ‡Ί Je, una kipaji katika sanaa za mitaani au michezo ya kisasa? Hii ni nafasi yako ya kushiriki katika KARDO International Street Culture & Sport Competition 2026 itakayofanyika Vladivostok, Urusi. Mashindano yanajumuisha: Hip-Hop Breaking (Breakdance) Graffiti DJing Parkour Freerunning Street Workout / Calisthenics Tricking Skateboarding BMX Kick Scootering Rollerblading (Inline Skating)

Mahitaji ya Kujiunga

Mahitaji ya Kujiunga
Jaza fomu ya maombi kupitia https://kardoaward.com.
Toa taarifa sahihi zinazohitajika.
Ambatisha nyaraka au vielelezo vinavyotakiwa na waandaaji (ikiwa vinahitajika).
Hakikisha unatuma maombi kabla ya tarehe 25 Julai 2026.

Masharti ya Kustahiki

Masharti ya Kustahiki
Awe kijana wa Kitanzania.
Awe na kipaji katika mojawapo ya fani zinazoshindanishwa.
Awe tayari kushiriki katika mashindano ya kimataifa.
Atimize masharti yaliyowekwa na waandaaji kupitia tovuti rasmi.

Faida na Manufaa

Faida na Manufaa
Fursa ya kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya kimataifa.
Kukutana na washiriki kutoka mataifa mbalimbali.
Kujenga mtandao wa kimataifa wa wasanii na wanamichezo.
Kuonyesha kipaji mbele ya majaji na wadau wa kimataifa.
Kupata uzoefu, kujifunza mbinu mpya na kuongeza ushindani katika taaluma yako.
Fursa ya kutambulika kimataifa kupitia jukwaa la KARDO