Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)
Mkopo wa Mfuko wa Maendeleo ya Vijana 2026 | Fursa za Vijana | UVCCM

Mkopo wa Mfuko wa Maendeleo ya Vijana 2026

Mikopo Muhimu Maombi yameisha
87
Wameona
Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana (OR–MV)
Shirika
Tanzania
Mahali

Maelezo ya Fursa

Mfuko wa Maendeleo ya Vijana umeanzishwa kwa lengo la kuwawezesha vijana kiuchumi kwa kuwapatia mitaji itakayowawezesha kuanzisha au kuendeleza shughuli mbalimbali za uzalishaji, biashara na utoaji wa huduma. Programu hii inalenga kuongeza ajira kwa vijana, kukuza ujasiriamali na kuchochea maendeleo ya uchumi wa Taifa.
Dirisha la kupokea maombi limefunguliwa rasmi. Vijana wote wenye miradi au mawazo ya miradi wanakaribishwa kutuma maombi. Sifa za Mwombaji: 1.Awe raia wa Tanzania, umri 18–35. 2.Awe na Kitambulisho cha Taifa (NIDA) au Namba ya NIDA. 3.Awe kwenye eneo linalotambuliwa kwa ajili ya biashara (mfano soko). 4.Awe mkazi wa eneo husika na awe na barua ya uthibitisho kutoka Serikali za Mitaa/Kijiji. 5.Awe mtu mmoja, kampuni changa au Kikundi cha Kijamii kilichosajiliwa kinachofanya shughuli ya kiuchumi. 6.Awe na andiko la mradi/biashara inayoiomba mkopo. 7.Awe na akaunti ya benki au namba ya simu iliyosajiliwa kwa jina la mwombaji.

Mahitaji ya Kujiunga

Nyaraka Zinazohitajika:
1.Andiko la mradi lisizidi kurasa 5
2.Kitambulisho cha Taifa / NIDA / Mpiga Kura
3.TIN (utambulisho wa mlipa kodi)
Leseni ya biashara (ikiwa ipo)
4.Barua ya uthibitisho wa eneo kutoka Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa/Kijiji
5.Picha mbili za mwombaji (zilipigwa ndani ya miezi 3)
6.Muhtasari wa kikao kilichosainiwa na wanachama wa kikundi (ikiwa ni kikundi)

Masharti ya Kustahiki

Namna ya kuomba Mkopo, Mwombaji atatuma barua ya maombi ikibainisha:
1,Jina la kikundi au mwombaji.Aina ya 2.mradi unaopendekezwa
3.Kiasi cha mkopo kinachohitajika
4.Mahali mradi utakapotekelezwa

Nyaraka Zinazohitajika:
1.Andiko la mradi lisizidi kurasa 5
2.Kitambulisho cha Taifa / NIDA / Mpiga Kura
3.TIN (utambulisho wa mlipa kodi)
Leseni ya biashara (ikiwa ipo)
4.Barua ya uthibitisho wa eneo kutoka Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa/Kijiji
5.Picha mbili za mwombaji (zilipigwa ndani ya miezi 3)
6.Muhtasari wa kikao kilichosainiwa na wanachama wa kikundi (ikiwa ni kikundi)

Faida na Manufaa

Faida na Manufaa:
1.Kupata mkopo wa kuanzisha au kuendeleza mradi
2.Kukuza ujasiriamali
3.Kutoa ajira kwa vijana
4.Kuchochea maendeleo ya uchumi wa Taifa